Thursday, March 30, 2017
NI FURAHA KUWA NA RAFIKI
Ishi na rafiki kwa akili kubwa mpe nafasi sababu katika siku usiyoidhania anaweza kuwa adui mkubwa sana kwako,Wakati huo huo ishi na adui kwa akili sababu huwezi jua kuna siku anaweza kuwa rafiki yako.
Wednesday, April 13, 2016
HABARI KWA UFUPI
Siku moja baada ya
aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Anne kilango kuvuliwa uongozi kwa kutosema
ukweli,Mkuu wa wilaya ya kishapu Hawa Nghubi ameiruka taarifa ya kutokuwepo kwa
watumishi hewa ambayo amesema ilimshtua alipoiona kwenye televisheni.
Tuesday, April 12, 2016
LA KWETU CONCERT NI TAMASHA KUBWA NA LA KIHISTORIA LINAKUJA KUTIKISA TANZANIA
Tamasha la LA KWETU CONCERT ni Tamasha kubwa na la kihistoria linakuja kupinga mauaji ya ndugu zetu Albino,na uzinduzi wake utafanyikia Mwanza na hivyo kuweza kuzunguka kanda ya ziwa yote na hatimaye kuzunguka nchi nzima.
Monday, April 20, 2015
HABARI KWA UFUPI
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameitaka jumuiya ya albino nchini
kuisukuma Serikali ili Rais Jakaya Kikwete asaini utekelezaji wa hukumu ya
kuwanyonga wauaji wa albino.Kauli ya Lowassa imekuja wiki moja tu baada ya Rais
Kikwete kusema hajapelekewa majina ya watu 16 waliohukumiwa kifo kutokana na
mauaji ya albino kutokana na mlolongo mrefu wa kisheria uliopo kabla ya
kumfikia.
Friday, April 17, 2015
HABARI KWA UFUPI
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana
kilizindua mkakati wake wa ushindi “Hakuna kulala, hakuna kula mpaka kieleweke”
katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kwa kufungua mafunzo yatakayoendeshwa nchi nzima
kwa viongozi wa vyama na Serikali za Mitaa
Wednesday, April 08, 2015
POLISI MWINGINE AUA MTU MWEUSI MAREKANI
Wakuu katika jimbo la South Carolina nchini Marekani wamemhukumu Afisa mmoja wa polisi mweupe, kwa kosa la mauaji.
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumpiga risasi raia mmoja mweusi na kumuuwa.
Picha ya Video ya kilichofanyika imewekwa mtandaoni.
Mkanda huo wa video unaonesha mtu mmoja kwa jina, Walter Scott, akipigwa risasi alipokuwa akimkimbia afisa huyo.BBC
Monday, March 30, 2015
Subscribe to:
Posts (Atom)