Pages

Tuesday, June 10, 2014

HABARI KWA UFUPI




Mgonjwa aliyepooza nusu mwili ambaye alikuwa amelazwa Hospitali ya Rufani Bugando Mwanza, amejikuta katika hali ngumu baada ya kuruhusiwa kurudi nyumbani akiwa na kidonda kikubwa sehemu ya makalio kilichotokana na kulala kwa muda mrefu kitandani bila kugeuzwa.Joseph Luhogola (38), ambaye amepooza mwili kuanzia usawa wa kifua hadi miguuni, amelazimika kwenda kwa mganga wa Kienyeji kutumia miti shamba kutibiwa ugonjwa unaomsumbua.


Siku chache baada ya kusambazwa picha za ngono zikiwahusisha baadhi ya wabunge katika mitandao ya kijamii, serikali imesema inawasaka waliozisambaza kwa kuwa ina uwezo wa kuwabaini.Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, alitoa kauli hiyo jana bungeni baada ya Spika Anne Makinda, kumtaka azungumzie picha chafu za baadhi ya wabunge zilizotolewa na kusambazwa kwenye mitandao.

Mfumuko wa bei wa taifa umeongezeka na kufikia asilimia 6.5 kutoka asilimia 6.3 Aprili mwaka huu, huku chanzo kikiwa ni upandaji wa bidhaa na huduma.Farihisi za bei nazo zimeongezeka hadi sh 149.89 Mei mwaka huu kutoka sh 140.76 Mei mwaka jana, huku bidhaa za vyakula na vinywaji baridi zikipanda bei kwa asilimia 8.5 Mei mwaka huu kutoka asilimia 7.8 Aprili mwaka huu.

Wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Boko Haram wamewateka nyara wanawake 20 kutoka jamii inayohamahama Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.Wanawake hao walichukuliwa katika Makazi ya Gakini Fulani karibu na mji wa Chibok ambako zaidi ya wasichana wanafunzi 200 walitekwa nyara Aprili, mwaka huu.

Viongozi wa kimataifa wanakutana jijini London kwa wiki nzima, kwa kongamano la kumaliza dhulma za kimapenzi katika mataifa yanayokabiliwa na mizozo.Mkutano huo, wa siku nne umeandaliwa na Waziri wa masuala ya nchi za kigeni wa Uingereza, William Hague na muigizaji maarufu na mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa, Angelina Jolie.

Mazoezi yanaweza kusaidia kupona baada ya kuugua saratani ya matiti lakini ni wanawake wachache sana wanashiriki katika mazoiezi, utafiti unasema.Watafiti wa Marekani, katika ripoti waliyochapisha katika jarida linaloandika mambo ya saratani,wanasema kuwa inajulikana wazi kwamba kufanya mazoezi ya aina moja au nyingine kunasaidia lakini imegunduliwa kuwa wanawake hawapendi kufanya mambo yanayowachosha.

No comments:

Post a Comment