Pages

Thursday, October 23, 2014

HABARI KWA UFUPI



Rais Jakaya Kikwete amesema endapo mipango yote itakwenda kama inavyoandaliwa, Watanzania wataipigia kura ya maoni Katiba Inayopendekezwa Aprili mwakani.Kauli hiyo ya Rais Kikwete aliyoitoa jana alipokutana na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Jamhuri ya Watu wa China, inapingana na ile ya Mwanasheria Mkuu wa Tanzania (AG), Jaji Frederick Werema ya hivi karibuni kwamba kura hiyo ingefanyika Machi 30, mwakani.


Wauguzi wa Zahanati ya Kurugee katika Kijiji cha Bulaga wilayani hapa wanalazimika kutumia chemli wodini wakati wa kuwahudumia wagonjwa kutokana na kukosekana kwa umeme.Mganga wa zahanati hiyo, Micoruah Simion alimwambia meneja wa mkoa wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mara, Henry  Byabato, kuwa awali walikuwa wakitumia karabai ambazo kwa sasa zimeishiwa gesi na halmashauri ya wilaya haijatoa fedha za kununulia gesi nyingine mpaka sasa.

Dar es Salaam. Matukio ya ujambazi yanaendelea kutikisa Jiji la Dar es Salaam baada ya watu wanaoaminika kuwa majambazi kumjeruhi kwa kumpiga risasi mkazi wa Kibaha, Nyalinga Steven na kumpora kiasi cha Sh15 milioni jana.

Mwanajeshi mmoja ameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa nje na ndani ya Bunge la Canada mjini Ottawa katika tukio linalodhaniwa kuwa la kigaidi,ambapo mji huo mkuu upo chini ya ulinzi mkali wa Polisi na wanajeshi.

Shirika la afya duniani leo linaongoza mkutano wa kamati yake ya dharura , kutathmini hali ya hivi karibuni kuhusiana na mlipuko wa Ebola .Mkutano huo unafanyaika wakati ugonjwa huo ukiendelea kuenea katika nchi tatu zilizoathiriwa zaidi na ugonjwa huo Guinea, Sierra Leone na Liberia - ingawa Senegal na Nigeria, ambazo zilikuwa na visa vichache zimetangazwa kutokuwa na ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment