Pages

Friday, October 24, 2014

HABARI KWA UFUPI




Wabunge wa Bunge la Muungano, wanakabiliwa na ukata baada ya Ofisi ya Bunge kushindwa kuwalipa posho zao tangu walipoanza vikao vya Kamati za Bunge, jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Ardhi na Maendeleo na Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, amesema atahakikisha ardhi inayochukuliwa na Shirika la Nyumba nchini (NHC) kwa ajili ya utekelezaji wa miradi haipatwi na migogoro baina ya shirika hilo na wananchi.

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeitaka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi maalum wa sh bilioni 17 kwa Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Daktari wa Marekani aliyekuwa akiwahudumia wagonjwa wa Ebola Nchini Guinea amepimwa na kukutwa na virusi vya ugonjwa huko katika hospitali ya ya mjini Newyork.Dr Craig Spencer ambaye ni mmoja kati ya madaktari wasio na mipaka alianza kujisikia maumivu na homa siku chache tu baada ya kurejea Marekani akitokea Afrika Magharibi.

Serikali nchini Nigeria inasema inachunguza taarifa ya idadi kubwa ya wanawake na wasichana waliotekwa nyara na wanamgambo wa Boko Haram Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo, pamoja na kwamba tangazo la kusitisha mapigano lililotolewa na majeshi ya serikali.

Viongozi wa Muungano wa Ulaya wanaokutana mjini Brassels wamefikia mkataba muhimu kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ambapo wameazimia kupunguza kiwango cha asilimia arobaini ya gesi chafu kufikia mwaka 2030 ikilinganishwa na viwango vya mwaka 1990 .

No comments:

Post a Comment