Pages

Sunday, June 01, 2014

SOMA HABARI KWA UFUPI

Kitendo cha wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuamua kuzima hoja ya kutaka kuunda Kamati Teule ya Bunge, kuchunguza kashfa ya ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Escrow iliyofunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kimekiweka chama hicho tawala kwenye wakati mgumu, Tanzania Daima Jumapili limebaini.Habari zinasema kuwa msimamo wa kukataa uundwaji wa kamati teule uliwekwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati wa kikao cha ndani cha wabunge wa chama hicho.


Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amerejesha fomu ya kugombea tena nafasi ya Katibu Mkuu wa chama hicho huku akisisitiza msimamo wake wa kuendelea kuwaunganisha Wazanzibari.Akikabidhi fomu hiyo kwa Katibu wa CUF Wilaya ya Magharibi Unguja, Juma Rajab, juzi, Maalim Seif alisema suala la ubaguzi kamwe halitopewa nafasi ndani ya chama hicho.

Maelfu ya polisi pamoja na wanajeshi wamepelekwa katika mji mkuu wa Thailand Bangkok kwa jaribio la kuangamiza maandamano dhidi ya mapinduzi ya kijeshi ya mwezi jana.Baadhi ya vituo vya treni pamoja na maduka ya jumla yamefungwa kutokana na maandamano hayo.Mwandishi wa BBC mjini Bangkok amesema kuwa eneo la biashara katikati ya mji huo limesalia kuwa mahame baada ya jeshi kulifunga.

Serikali ya Tunisia imefutilia mbali mkutano wa dharura wa mataifa ya kazkazini mwa Afrika ili kuzungumza kuhusu mzozo wa kisiasa nchini Libya.Msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni nchini Tunisia Mokhtar Chao-uachi amesema kuwa wameshindwa kupata mtu atakayeiwakilisha serikali ya Libya kufuatia makabiliano ya mamlaka katika serikali hiyo.
 

No comments:

Post a Comment