Polisi kaskazini mashariki mwa Nigeria wanasema kuwa shambulizi la bomu limewauwa zaidi ya watu 14 na kuwajeruhi wengine wengi.
Ripoti zimesema kuwa mlipuko huo uliotokea
katika mji wa Mubi, ulilenga chumba kimoja cha burudani ambako watu
walikuwa wakitazama mechi ya soka kwenye televisheni.
Katika
miezi michache iliyopita, Boko Haram wamezidisha mashambulio yao hasa
kaskazini mashariki mwa
Nigeria. Mamia ya watu wameuawa na wengine wengi
kujieruhiwa. Pia wameshambulia nyumba za watu na kuzichoma moto, na
kisa kilicho tikisa jamii ya kimataifa ni wasichana zaidi ya 200
waliotekwa nyara yapata miezi miwili sasa hadi leo hawajulikani waliko.
Uharibifu uliozidi
Mashambulio haya yameacha uharibifu mkubwa. Waliosalimika wamelazimika kukimbia makwao huku shule zikiachwa bila wanafunzi.
Shambulio hilo limetokea karibu na mpaka kati ya
Nigeria na Cameroon katika jimbo la Adamawa-mojawepo ya majimbo ambako
sheria ya hali ya hatari inatumika kutokana na mashambulizi ya kundi la
waislamu wenye itikadi kali la Boko Haramu.
Katika mwezi mmoja pekee watu zaidi ya 200 wameuawa katika mji huo.
Lakini sasa katika maeneo mengine ya kaskazini
ambako inasemekana usalama umerejea kiasi, kama vile mji wa Kano juhudi
zinafanywa kung'oa mizizi ya uovu huo.
Wanamgambo wa kiislamu AL shabaab wanaodaiwa
kuwa na uhusiano na AL qaeda wamekuwa wakiwazuia wananchi kushiriki
mambo yanayohusishwa na Mataifa ya magharibi. Inakisiwa kuwa zaidi ya
wanafunzi milioni 11 kaskazini mwa Nigeria hawapewi mafunzo mengine
yoyote mbali na ya kidini.
Wanafunzi waathirika
Mashirika ya kijamii hasa kutoka Uingereza yamekuwa yakifadhili
kupitia taasisi za nchini humo masomo ya ziada hasa katika shule za
mafunzo ya kidini, ili yatoe elimu ya ziada mbali na Qurani. Tayari
maelfu ya wanafunzi wanafaidi lakini bado kuna wengi zaidi wanaotishiwa
usalama wao na inadaiwa ni kiasi kikubwa zaidi ya nchi hiyo haiwezi
kufikiwa.
Licha ya mauaji ya miaka mingi yaliyofanywa na
kundi hilo la Boko Haram na hata kujitangaza hadharani uhusiano wao na
kundi la AL Qaeda, ni wiki iliyopita tu ambapo Umoja wa Mataiifa
umeilitangaza kuwa kundi la kigaidi.
Japo wengi wanaona kuwa hatua hiyo imechelewa,
bado inatoa matumaini ya kuweza kuchukuliwa hatua zaidi kusaidia
kukabiliana na kundi hilo.BBC
No comments:
Post a Comment