Mkuu wa tume ya haki za binadamu wa umoja wa mataifa Navi Pillay
Kamishna wa tume ya Umoja wa Mataifa ya haki za
binadamu ametoa taarifa za kutisha na kuhuzunisha kuhusu ghasia za hivi
karibuni katika Jamuhuri ya Afrika ya kati , baada ya kutembelea taifa
hilo kwa siku tatu .
Navi Pillay amesema watoto katika taifa hilo
wamekuwa wakikatwa katwa vipande na wauaji wamekuwa wakila nyama ya watu
wanao wauwa.
Aliongeza kusema kuwa chuki baina ya jamii zimefikia kiwango cha kutisha, na kwamba watu wamekua wakiteswa na kuchomwa .
Hata hivyo amesema kupelekwa huko kwa vikosi vya Ufaransa na Afrika kumepunguza kiwango kikubwa cha mauaji kwa sasa.
Jamuhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika limbo la ghasia baada ya waasi kuchukua mamlaka mwezi Machi mwaka jana. BBC
No comments:
Post a Comment