Bunge la Tanzania mjini Dodoma
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete leo anatarajiwa
kuzindua rasmi shughuli za bunge la kitaifa kuhusu marekebisho ya katiba
mjini Dodoma katika hatua itakayoanzisha rasmi mjadala wa kitaifa
kuhusu marekebisho hayo.
Bunge hilo maalum la katiba limepewa kati ya
siku 70 hadi 90 kujadili rasimu ya katiba na kisha kuifanyia marekebisho
kabla ya kura ya maamuzi.
Kuna ripoti kwamba baadhi ya wajumbe kutoka upinzani na mashirika ya kiraia yanapanga kuvuruga shughuli hiyo ya uzinduzi.
Suala la hotuba ya Rais Kikwete limekuwa sehemu
ya mjadala katika Bunge hilo kutokana na baadhi ya wajumbe kuhoji sababu
za Jaji Warioba kuwasilisha Rasimu kabla ya Rais kuzindua Bunge kwa
mujibu wa kanuni.
Mjadala huo uliwafanya baadhi ya wajumbe kumzuia
Jaji Warioba Jumatatu iliyopita kuwasilisha rasimu hiyo kama ilivyokuwa
imepangwa.
Kikao cha maridhiano kilifanyika siku hiyohiyo
usiku na kufikia mwafaka kwamba Mwenyekiti huyo wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba awasilishe Rasimu ndiyo Rais aweze kuzindua shughuli ya
kujadili rasimu hiyo kabla ya kura ya maoni.
No comments:
Post a Comment