Pages

Monday, March 24, 2014

SOMA HABARI KWA UFUPI




Naibu Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni, Juma Nkamia,ametishia kuvifungia au kuvifuta vyombo vya habari vitakavyo wachafua watu,serikali na kuhatarisha usalama wan chi aliyasema hayo jana katika tamasha la voice of youth lililokuwa likijadili mambo mbalimbali yanayohusu vijana.
                              **********************
Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, kukosoa hatua ya Rais Jakaya Kikwete kutoa maoni yake kuhusu rasimu ya Katiba, kimekosolewa.
Pia, imesisitizwa kuwa hakukosea kufanya hivyo na kwamba hotuba yake, haikuvuruga wala kuingilia mchakato ulio bungeni.
                            **********************

Wasichana waliotekwa nyara na kundi lenye itikadi kali za kidini, Boko Haram nchini Nigeria, wameielezea BBC ukatili walio upitia mikononi mwa kundi hilo.Wakati wakizuiwa, wasichana hao walishuhudia watu kadhaa wakiwemo baadhi wanaotoka kijiji kimoja na wapiganaji wa kundi hilo, wakikatwa shingo.
                            ***********************
Mzozo kuhusu Crimea na Ukraine utajadiliwa leo na viongozi wa mataifa mbalimbali akiwemo rais Obama. Viongozi hao wamejumuika katika kongamano la kujadili usalama wa nyuklia lakini ajenda hio inatarajiwa kugubikwa na mazungumzo kuhusu hatua ya Urusi kunyakua eneo la Crimea.



No comments:

Post a Comment