Mkurugenzi
wa uendeshaji wa shirika la world Vision Tanzania.Dk Yoshi Kasilima
ameshauri wafanyakazi wa afya wa Afrika mashariki na kati kujengewa
uwezo na utangamano zaidi katika ngazi ya jamii.Aliyasema hayo katika mkutano
wa wadau wa afya kutoka kanda ya maziwa
makuu.Dr Kasilima alisema Tanzania ,Kenya,Uganda na Rwanda zinatakiwa
kuwajengea uwezo wafanyakazi wa afya katikangazi ya jamii.
Wazazi katika kaunti ya Kirinyaga mkoa wa Kati nchini Kenya wameandamana kwa hasira baada ya mwalimu kumchapa mtoto mmoja wa shule ya msingi hadi akafariki.Mtoto huyo inaarifiwa alichapwa kichwani na mwalimu na kuzirai. Alifariki alipokuwa anapelekwa hospitalini.
Waziri mkuu wa Malysia Najib Razak amewasili jijini Perth,magharibi mwa Australia ambako shuguli za kutafuta ndege ya MH370 inaendelea ili kuwashukuru wale wote wanaohusika na shuguli za kusaka ndege ya malysia iliyotoweka majuma matatu yaliyopita.
No comments:
Post a Comment