Mkuu wa Mkoa wa
Pwani, Mwantumu Mahiza anadaiwa kuhamisha gari la wagonjwa kutoka Kituo cha
Afya cha Kibiti kwenda Zahanati ya Nyamisati kwa ‘shinikizo la wakubwa’.Gari hilo
lililotolewa na Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) kwa Kituo cha Afya Kibiti kwa
ajili ya kusaidia wakazi wa maeneo hayo na jirani, lakini Mahiza aliagiza
lihamishiwe Nyamisati ambako inadaiwa wanatoka “watu wazito wenye ushawishi
mkubwa”.
Bomu
lililolipuka katika mji wa Kano kaskazini mwa Nigeria limewaua watu 5 na
kuwajeruhi wengine wengi.Shambulio hilo limefanywa katika eneo linaloaminiwa
kuwa na waumini wengi zaidi wa dini ya kikristu, ambao wamekuwa wakilengwa mara
nyingi na wapiganaji wa Boko Haram.
Tahadhari
zaidi zimetolewa nchini Kenya za kutokea mashambulio katika baadhi ya maeneo ya
umma na foleni za barabarani.Mitandao ya kijamii ya twitter na face book
imetumiwa kusambaza ujumbe miongoni mwa wananchi kutoa tahadhari hiyo.
Serikali
ya Libya imesisitiza kuwa bado imedhibiti uongozi wa nchi.Hii ni hotuba ya
kwanza kutoka kwa serikali hiyo tangu kutokea mapigano katika mji mkuu Tripoli
siku ya Jumapili.Maafisa wanasema kuwa watu 2 wameuawa na wengine zaidi ya 55
kujeruhiwa katika mapigano hayo ambayo ni ya punde zaidi.
No comments:
Post a Comment