Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), imepandisha gharama
za huduma hospitalini hapo na sasa mgonjwa atakayelazwa atalazimika kulipa
Sh5,000 kwa siku.Gharama hizo zitalipwa kwa wagonjwa wote wa rufaa, ilisema
taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo, Dk Marina
Njelekela na kusambazwa kwenye vyombo vya habari.
Suala la uhaba wa dawa na vifaa tiba katika hospitali nchini
ikiwamo Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, limeonekana kuielemea Wizara ya Afya
baada ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid kuthibitisha, huku
akidai kuwa Serikali itapeleka fedha kwa awamu Bohari ya Kuu ya Dawa ili
kupunguza uhaba huo.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon amezitaka nchi
duniani kuacha tabia ya unyanyapaa kwa madaktari na manesi waliofanya kazi
katika nchi zilizoathiriwa na ugonjwa wa Ebola na kuwalazimisha kwenda
karantini pindi warejeapo nyumbani.
Ripoti mpya iliyotolewa inaonesha kuwa nchi za SCANDNAVIA
zinaongoza kwa uwiano wa kijinsia.Katika ripoti yake ya mwaka iliyoitoa Jukwaa
la kiuchumi duniani limeangalia fursa kwa wanawake katika nchi 142. Huku nchi
za Afrika, zikiongozwa na Rwanda.
Mahakama nchini Saudi Arabia imetoa hukumu ya kifungo cha
miaka mitano mpaka nane kwa wanasheria wa tatu nchini humo, kwa kosa la kukosa
mfumo wa haki za nchi katika mtandao wa kijamii blogs na twitter.
No comments:
Post a Comment