Watu wasiojulikana wamewanyonga
hadi kufa ndugu wawili wakazi wa maeneo ya Mtaa wa Madafu, Tandika jijini hapa.Ndugu
hao, Mwakamu Mariamu Buruhani (39) na Nuru Tumwanga (42) walinyongwa usiku wa
kuamkia jana.
Mawaziri katika Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wameanza kampeni kuwataka wananchi kuunga
mkono Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa wakisema imezingatia masilahi ya
Zanzibar kiuchumi na kiutawala.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
CCM, Nape Nnauye amesema hatua ya viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba
ya Wananchi (Ukawa), kuingia katika makubaliano ya kushirikiana “ni kaburi la
vyama hivyo.”Wakati Nape akisema hayo, baadhi ya wasomi wamesema ni hatua kubwa
lakini yenye kuhitaji kuwa na sera na itikadi ya pamoja.
Watoto 30 wametekwa nyara na watu
wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram.Watoto hao wametekwa nyara kaskazini
mashariki mwa Nigeria. Tukio hili linakuja siku chache baada ya kundi hilo
kuwateka wanawake na wasichana kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Ni miezi sita sasa baada ya
wanamgambo wa kiislam wa kundi la Boko Haram kuwateka wanafunzi wasichana Zaidi
ya 200 kaskazini mashariki mwa Nigeria, wasichana watatu ambao wametoroka
wamezungumza katika mahojiano maalum na idhaa ya Kihausa ya BBC.
No comments:
Post a Comment