Rais Jakaya Kikwete
amelikata Jeshi la Polisi nchini kujiandaa kikamilifu ili kukabiliana na vurugu
zozote zitakazojitokeza wakati wa uandikishaji wapigakura, upigaji Kura ya
Maoni ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka
huu.
Mwanamuziki mwenye uwezo na mvuto jukwaani, Juma
Nature amesema kuwa hana mpango wa kugombea ubunge katika Jimbo la Temeke mwaka
huu, licha ya awali kutangaza nia hiyo.Nature ametoa kauli hiyo huku wasanii
wengine wakitangaza nia ya kuwania ubunge majimbo mbalimbali.
Wakati joto la mbio
za kuwania urais likiendelea kuisisimua nchi, Umoja wa Wanawake Wanasiasa
Tanzania (Ulingo), kwa kushirikiana na Mtandao wa Wanawake na Katiba, umesema
tayari wameandaa majina matano ya wanawake kuwania nafasi hiyo baadaye mwaka
huu.
Waziri mkuu wa
Uingereza, hataendelea tena na wadhfa wake huo, iwapo atarudi madarakani katika
uchaguzi mkuu wa mwezi Mei.David Cameron, ameiambia BBC kuwa, anadhani awamu ya
tatu inaweza kuwa ni kipindi kirefu kwake kukaa madarakani na kiongozi mpya ni
vizuri kuchaguliwa.
Raisi Barack Obama
ametoa mwito kwa wa Nigeria kusitisha vurugu hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa
nchi hiyo mapema mwishoni mwa wiki hii.Wasi wasi wa hali ya usalama umezidi
kuongezeka nchini humo wakati siku ya kupiga kura kadiri inavyokaribia ambapo
wananchi wa Naijeria wanatarajiwa kupiga kura jumamosi wiki hii baada uchaguzi
huo kuhairishwa mwezi uliopita kutokana na mashambulio ya kundi la Boko Haram.
No comments:
Post a Comment