Je unamkumbuka mwanamuziki wa kufoka Andre Johnson
ambaye alikata Uume wake mwezi Aprili na kisha kujirusha kutoka juu ya
jumba moja mjini Los Angeles?
Sasa basi emetoa sababu zake akisema alikuwa na akili timamu alipokuwa anafanya hivyo.
Johnson,
aliishangaza jamii ya wanamuziki wa kizazi kipya, kufuatia kitendo
chake cha kukata uume wake Kaskazini mwa Hollywood mwezi Aprili.
Madaktari walishindwa kunguanisha sehemu aliyoikata na sehemu nyeti ya
mwili wake.
Tangu hapo alikimya kwa miezi miwili akipokea matibabu.
Lakini aliamua wiki hii kujieleza kwa nini
alichukua hatua hiyo na kuambia kituo cha televisheni cha E! nchini
Marekani:''Ndio nilikuwa nimetumia dawa za kulevya , lakini nilikuwa
najifahamu.''
'Mimi sio mwanadamu'
Nilikata sehemu yangu ya siri kwa sababu hiyo
ndiyo ilikuwa chanzo cha masaibu yangu. Suluhu langu kwa masaiibu yangu
ni kwamba nimeelewa kuwa kitendo cha ngono ni cha mwanadamu, mimi sio
mwanadamu, 'mini ni mungu''.......''vitendo vya ngono viliniingiza
katika matatizo mengi. Mimi siko hapa ardhini kama mwanadamu bali mungu
''
Matamshi yake Johnson, yanaonekana kama ya mtu
anayekabiliwa na matatizo ya kiakili, lakini Johnson anasisitiza kuwa
yuko timamu , yeye sio kichaa.
Alisema amekuwa akipata matibabu ya kisaikolojia lakini daktari alimwambia hana matatizo.
''Watu wananiona kama mimi ni mwendawazimu, kwa hivyo sikutaka kuongea sana kuhusu swala hilo. ''
"sikutaka kujiua ,'' alisema Johnson.''
"hilo ndilo jibu langu kwa kitendo
nilichokifanya. Leo nafurahi niko hai, na hilo ndilo jambo muhimu zaidi,
hata bila ya uume wangu. ''BBC
No comments:
Post a Comment