Siku moja baada ya
aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Anne kilango kuvuliwa uongozi kwa kutosema
ukweli,Mkuu wa wilaya ya kishapu Hawa Nghubi ameiruka taarifa ya kutokuwepo kwa
watumishi hewa ambayo amesema ilimshtua alipoiona kwenye televisheni.
Ripoti ya utafiti
kuhusu ujangili wa meno ya Tembo imebaini kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi
mbili za Afrika ambazo idadi kubwa ya Tembo wanauawa.Utafiti huo wa njia ya
vinasaba (DNA)uliofanywa na shirika la umoja waMataifa ya kupambana na Dawa za
kulevya na uhalifu(UNODC),Benk ya Dunia (WB)na Shirika la polisi la Kimataifa
(Interpol)ulibaini kuwa asilimia 85 ya meno ya tembo yanayokamatwa asilia yake
ni mbuga za Selous,Ruaha na Ruangwa, Tanzania.
Waasi nchini Sudan
Kusini wanasema kuwa wanachama wake 16 wa kitengo cha habari, wamekamatwa na
kupigwa vibaya na maafisa wa usalama katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba.Kundi
hilo la waandishi wa habari lilikuwa limetanguliwa katika mji mkuu wa Juba,
siku kadhaa kabla ya kuwasili kwa kiongozi wa waasi Dkt Riek Machar.
Mawakala kutoka
afisi ya mkuu wa sheria nchini Panama wamevamia jengo la kampuni ya mawakili ya
Mossack Fonseca, kutafuta ushahidi wowote unaohusiana na biashara haramu.Kampuni
hiyo imeshutumiwa kwa kuepuka kulipa kodi na ulaghai lakini mwanzilishi wake
Ramon Fonseca amesema kuwa operesheni zake zote ni halali.
Muungano wa ulaya
umelaani hatua ya rais wa Macedonia, Gjorge Ivanov, kuwasamehe wanasiasa
waliohusishwa na ufisadi.Kamishna anayehusika na upanuzi wa muungano huo
Johannes Hahn, amesema kuwa msamaha huo hauambatani na uelewa wake wa sheria na
hivyo, unahatarisha azma ya Macedonia kuwa mwanachama wa muungano huo.
No comments:
Post a Comment