Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni jana ilimlipua mbunge kutoka kambi yao, Zitto Kabwe
ikimhusisha na ufisadi wa Sh119 milioni kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF) na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa).
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ameuagiza uongozi na wananchi wa wilayani hapa
mkoani Manyara kumbana Mwenyekiti wa Chadema wa wilaya, Augustino Mayomba
anayedaiwa kumiliki hati ya mkataba wa mnara wa simu wa Vodacom uliopo Kijiji
cha Bassotu.
Ikulu
ya White House imeeleza masikitiko yake kuhusiana na wapiganaji waasi
wanaoungwa mkono na Urusi Mashariki mwa Ukraine kuwa wanatumia silaha kubwa
katika makabiliano nchini humo.
BBC
imebaini kuwa Kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wahamiaji wanaofika ulaya
katika miezi ya hivi karibuni.Kwa mujibu wa shirika la mpaka la Muungano wa
Ulaya Frontex, Idadi kubwa ya wakimbizi hao ni wale wanaojaribu kuvuka kutoka
kaskazini mwa Afrika wakielekea Italia.
No comments:
Post a Comment