Pages

Monday, May 05, 2014

SOMA HABARI KWA UFUPI



Tembo wanane katika Hifadhi ya Tarangire mkoani hapa wameuawa katika kipindi cha Novemba 2013 hadi sasa huku meno 17 ya tembo yakikamatwa katika operesheni inayoendelea kufanywa na askari wa hifadhi hiyo.Imeelezwa kuwa hiyo inaonyesha kwamba hali ya ujangili katika hifadhi mbalimbali nchini inaendelea na kusababisha kupotea kwa wanyama hao.


Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amezitaka taasisi binafsi kushirikiana na Serikali katika kampeni ya kutokomeza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi nchini.Akizindua kampeni ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha Sh 1.5 bilioni zitakazotumika kusaidia kutokemeza maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na ukimwi, Rais Kikwete alisema Ukimwi bado ni tishio.

Watu wawili wameuawa na wengine 60 kujeruhiwa kufuatia milipuko miwili katika mji mkuu wa Kenya Nairobi ambayo imelenga mabasi mawili ya abiria.Mabasi hayo yalilipuliwa katika eneo la barabara ya Thika karibu na mji mkuu. Mlipuko mmoja umetoa katika basi la abiria ambalo lilikua likisafirisha abiria kutoka mjini Nairobi katika barabara ya Thika ambayo kawaida ina shughuli nyingi.

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, amezungumza wazi kwa mara ya kwanza kuhusu kutekwa kwa waschana takriban 200 wa shule kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Katika taarifa yake ya kwanza hadharani tangu wasichana 200 kutekwa nyara na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Waislamu wenye itikadi kali wa Boko Haram, Rais Goodluck Jonathan, amesema kuwa kila juhudi zinapaswa kufanywa kuwakomboa wasichana hao.

No comments:

Post a Comment