Mbu jike aina ya Aedes Egyptiae ndiye anaeeneza ugonjwa huu wa Dengue
Ugonjwa wa homa ya dengue umezidi
kusambaa mkoani Dar es Salaam na sasa umeathiri wilaya zake tatu na kuzua hofu
kwa wananchi.
Ray C akiwa amelawazwa Hospital ya Mwananyamala
Miongoni mwa walioathiriwa na
homa hiyo mwanamuziki maarufu Rehema Chalamila (Ray C)ambaye amelazwa katika
wodi namba tano ya Hospital ya Mwananyamala.
Mmoja wa madaktari wa hospital
hiyo,alithibitisha kulazwa kwa Ray C kutokana na Ugonjwa huo jana.Mtaalamu
asema hali ni mbaya kuliko inavyodhaniwa,anasema zaidi ya asilimia 50 ya
wanaopimwa na kubainika ni watu wazima kuanzia miaka 18.Mbu aenezae ugonjwa huu
ni mweusi ni jike aina ya Aedes Egyptiae.
No comments:
Post a Comment