Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam,
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema, amemsamehe Askofu wa Kanisa la
Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye hivi karibuni alimtolea maneno makali
kutokana na kutofautiana naye juu ya msimamo wa viongozi wa Kikristo kuhusu
Katiba Inayopendekezwa.
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe ametoa wito kwa
vijana barani Afrika kupinga dhana ya ukoloni mamboleo pamoja na kulinda
rasilimali zilizopo ndani ya bara hili kwa masilahi ya vizazi vijavyo.Rais
Mugabe alitoa kauli hiyo juzi, wakati akizindua kongamano la tatu la viongozi
vijana Afrika linalofanyika hapa na kuhudhuriwa na zaidi ya washiriki 400
kutoka China na Afrika.
Mkuu wa Tume Huru ya
Uchaguzi nchini Nigeria amesema anatumaini kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa
rais nchini humo ifikapo Jumatatu jioni.Upigaji kura uliendelea katika siku ya
pili ya uchgaguzi baada ya kutokea hitilafu katika kadi za kielektroniki na
kuchelewesha usajili wa baadhi ya wapiga kura.
Idara ya usalama
nchini Brazil imesema kuwa imewaua watu saba waliokuwa wakifanya jaribio la
kupora katika benk moja na ambao pia wanadaiwa kujihusisha na dawa za kulevya.Taarifa
hizo zinasema kuwa majambazi hao walianza kurushiana risasi na Polisi katika
mji wa Novos Kaskazin Mashariki mwa Brazil.
Mazungumzo kuhusu
mpango tata wa Iran wa nyuklia yameendelea nchini Uswisi, kwa kuwasili mawaziri
wa mambo ya nje kutoka mataifa sita yenye nguvu duniani.Kiongozi wa mazungumzo
wa Iran Abbas Araqchi amesema makubaliano yanawezekana-- lakini mazungumzo yako
katika hatua ngumu na bado kuna mambo ya kutatua.
No comments:
Post a Comment