Pages

Wednesday, July 23, 2014

UNYAMA HUU MPAKA LINI "MSICHANA ABAKWA HADI KUFA"


Kinamama  walio karibu na familia ya marehemu Isabela Andrew aliyebakwa hadi kufa wakiangua kilio baada ya kushuhudia mahali mwili wake ulipokutwa huko Area C mjini Dodoma jana.  Na Mpigapicha Wetu 

Mfanyakazi wa ndani, Isabella Andrew (18), amefariki dunia na kifo chake kikidaiwa kusababishwa na kubakwa na watu wasiojulikana.


Mwili wa msichana huyo ulikutwa ukiwa umeharibika katika moja ya pagale, lililopo Area C, Dodoma Mjini na mwandishi wetu alishuhudia ukitolewa hapo kwa machela huku polisi wakiwahoji mashuhuda wa tukio hilo.


Mkazi wa Mtaa wa Kiwanja cha Ndege, Jackson Coy aliyekuwa akiishi na binti huyo alisema msichana huyo alipotea tangu Jumamosi iliyopita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime, alisema mwili huo uliokotwa jana saa mbili asubuhi na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo chake.

Mwili huo ulibainika baada ya mama mmoja, Rehema Msambile kufika katika pagale hilo alipokuwa akifuatilia nyendo za mtoto wake ambaye juzi alipigwa kwa tabia ya utoro shuleni.

“Niliamua leo (jana) kumfuatilia, nikaanza katika mapagale.
Nilipofika hapa ndipo nikaona mwili wa marehemu ikabidi nimuite jirani hapo aje aone,” alisema.

Diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege, Henry Kandenga alisema mazingira yanaonyesha kuwa binti huyo alibakwa kwa sababu walikuta nguo za ndani zikiwa pembeni.

“Hakuna yowe iliyosikika kwamba kuna mtu anauawa ukizingatia kwamba nyumba ziko jirani na hata nyumba aliyokuwa akiishi ni jirani na mahali alipokutwa,” alisema.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.Mwananchi

No comments:

Post a Comment