Watoto watatu wa familia moja wamefariki dunia baada ya kula futari
inayosadikiwa kuwa na sumu katika Kijiji cha Kwasunga, Wilaya ya Handeni
mkoani Tanga.
Akizungumzia tukio
hilo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Costantine Massawe alisema tukio
hilo lilitokea juzi saa tatu usiku, ambapo watoto hao wanatoka kwenye
familia ya Jumbe Waziri (40).
Alisema familia hiyo
ilikula futari hiyo akiwemo Waziri, wake zake wawili na watoto ambapo
wote walianza kujisikia vibaya, kukimbizwa katika Kituo cha Afya
kilichopo Mkata wilayani humo, lakini watoto hao walifariki dunia na
wazazi wao wamelazwa hospitalini hapo.
Aliwataja watoto hao
waliofariki kuwa ni Mwajuma Jumbe (3), Ramadhani Jumbe (5) na Abdi Jumbe
(7), ambapo baada ya wazazi wao kupata matibabu kituoni hapo,
waliruhusiwa kutokana Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili
kubaini chanzo cha vifo hivyo.
No comments:
Post a Comment