Waziri mkuu wa Libya Abdallah Al Thinni amekuwa akisisitiza
kuwa Serikali haikuamuru kuhusu shambulio hilo
Wizara ya afya nchini Libya imesema zaidi ya watu 40
wameuwawa mjini Benghazi siku Ijumaa katika mashambulizi anga na nchi
kavu yaliyoongozwa na kanali wa zamani wa jeshi dhidi ya wanamgambo wa
kiislam.
Vurugu hizo zilizofanyika zinaelezwa kuwa
zilikuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea tangu mapinduzi ya yaliyomuondoa
madarakani Kanal Muamar Gadafi mwaka 2011.
Taarifa kutoka mjini Benhgazi zinasema hivi sasa utulivu umerejea kwenye mji huo kama ilivyokuwa awali.
Mtu aliyeogoza mashambulizi hayo, Khalifa Haftar
amesema ataendelea na kampeni yake ya kuwaondoa watu wote aliowaita
magaidi nje ya mji wa Benghazi.
Serikali kuu imelaani matumizi hayo ya nguvu na kuuita hatua hiyo kama jaribio la mapinduzi lililoshindwa.BBC
No comments:
Post a Comment