Balozi wa Marekani nchini Kenya, Robert Godec,
amesema kuwa uchunguzi wao umebaini Kenya ipo katika hali ya hatari
kubwa ya kushambuliwa na magaidi.
Bwana Godec ametaka usalama uimarishwe katika ubalozi wa Marekani nchini humo na maeneo mengine ya nchi.
Bwana Godec amesema Marekani ipo tayari kufanya kazi na nchi ya Kenya kupiga vita ugaidi.
Taarifa hiyo ya balozi imetolewa baada ya
kutokea milipuko miwili siku ya Ijumaa katika soko moja jijini Nairobi
ambapo watu kumi na wawili walifariki dunia.
Wakati huo huo Shirika la Msalaba mwekundu limeendelea kutoa wito kwa
watu mbali mbali kuchangia damu kwa watu 86 waliojeruhiwa ambao
wamekuwa wakipata matibabu katika hospitali mbalimbali jijini Nairobi.
Baadhi ya viongozi nchini kenya wametaka sheria
ya ugaidi kurekebishwa ili washukiwa wa ugaidi wasiachiliwe kwa dhamana
katika mahakama za nchi hiyo.
Pia wamelaumu hatua za mataifa ya magharibi
zikiwemo Uingereza , Marekani na Australia kutoa tahadhari dhidi ya raia
wao kwenda nchini Kenya.
Tayari mamia ya watalii kutoka Uingereza
waliokuwa wamewasili mjini Mombasa wamerudi nyumbani baada ya onyo hilo
kutoka kwa serikali yao.
Wizara inayosimaia utalii nchini Kenya inasema ina mpango wa kufufua sekta ya utalii kufuatia mashambulizi hayo ya kigaidi.BBC
No comments:
Post a Comment