Serikali
imesisitiza uamuzi wake wa kupiga marufuku uingizwaji nchini wa kuku, nyama ya
kuku na vifaranga ili kudhibiti ugonjwa ya mafua ya ndege na kulinda wawekezaji
wa ndani.Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus Kamani alitoa agizo
hilo baada ya kutembelea kampuni ya Tanzania Poulty Farms Limited, inayomiliki
shamba la kuku wa nyama na vifaranga lililopo kijiji cha Ngogongare na kiwanda
cha uchinjaji kuku kilichopo Mbuguni wilayani Arumeru.
Mamia
ya watalii kutoka Uingereza waliokuwa kisiwani Mombasa Kenya wamelazimishwa
kurejea makwao baada ya serikali ya nchi hiyo kutoa tahadhari ya tishio la
mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya.Kampuni zinazopanga safari za watalii
kutoka Uingereza Thomson na First Choice zilifutilia mbali safari zote
zilizokuwa zimepangwa kuwaleta watalii Mjini Mombasa hadi mwezi Oktoba
zikihofia usalama wao.
Shughuli
ya kuhesabu kura imeanza rasmi nchini India baada ya uchaguzi uliodumu kwa
kipindi cha wiki tano.Matokeo ya awali yanaashiria ushindi kwa muungano
unaoongozwa na mgombea wa upinzani Narendra Modi aliayeahidi nafasi za ajira na
maendeelo ya kiuchumi.Kuna hali ya shangwe kwenye makao makuu ya chake cha BJP
mjini Delhi kulikowekwa televisheni kubwa zinazoonyesha matokeo huku pia nyimbo
zikiimbwa.
Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Luiz Felipe
Scolari,anatarajiwa kuchunguzwa na polisi kulingana na taarifa kutoka ncini
Portugal licha ya kocha huyo kukanusha madai kuwa alikwepa kulipa kodi.Bwana
Scolari alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Portugal kuanzia mwaka 2003 hadi
mwaka 2008. Madai hayo yanaonekana kuhusishwa na wakati wake alipokuwa nchini
humo.
Polisi
wa kupambana na ghasia wamefyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya maelfu ya
waandamanaji katika barabara za miji ya Sao Paolo na Rio de Janeiro walipinga
mfumuko wa gharama ya uenyeji wa kombe la dunia litakaloanza mwezi ujao nchini
Brazil.Baadhi ya waandamanji walipura mawe na kuchoma magurudumu ya magari na
kufunga mabarabara ya miji wakidai serikali haikuzingatia matakwa ya wananchi
kama vile elimu sekta ya afya na muundo msingi .
No comments:
Post a Comment