Wanasayansi nchini Ufaransa wamebaini kwamba virusi
vya Ugonjwa wa Ebola ndio chanzo cha ugonjwa wa homa ya haemorajic
nchini Guinea ambayo inaaminika kuwauwa karibia watu sitini.
Ugonjwa huo ambao unaweza kuambukizwa kwa haraka ulianza nchini humo yapata majuma sita yaliopita.
Dalili za ugonjwa huo ni kutoka damu,kuharisha pamoja na kutapika.
Afisa mmoja wa wizara ya afya nchini Guinea
amesema kuwa takriban visa vinane vya ugonjwa huo vimeripotiwa hususan
kusini mwa taifa hilo.
Amsema kuwa serikali ya taifa hilo inatumia kila njia kukabiliana na ugonjwa huo lakini inaendelea kushindwa.
Kufikia sasa hakuna tiba ya ugonjwa wa Ebola ambao husambazwa kupitia kugusana na walioambukizwa.BBC
No comments:
Post a Comment