Wakimbizi wa mapigano mashariki mwa Congo
Mili 25 imepatikana Ziwa Albert baada ya boti iliyokuwa imebeba wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuzama.
Wakimbizi hao walikua wakitoroka kutoka kambi ya wakimbizi ya Kyangwali wilayani Hoima magharibi mwa Uganda, wakirejea kwao.
Kwa sasa Jeshi la polisi linaendelea na jitihada
za kutafuta miili zaidi. Kamanda wa polisi wa eneo hilo John Ojukuna
amesema watu 43 wameokolewa. Boti iliyozama inadhaniwa kuwa ilikua
imebeba zaidi ya wakimbizi 100.
Wengi wa wakimbizi hao ni wale waliokimbia mapigano mashariki mwa Congo mwaka jana.
Mwendeshaji wa boti hiyo amekamatwa na jeshi la
polisi na inadaiwa kuwa alikua amelewa. Wakimbizi waliookolewa wameambia
polisi kuwa alikuwa mlevi na alikua akiendesha boti hiyo kwa kasi sana.
Hii sio mara ya kwanza ajali ya boti kuua watu
katika Ziwa Albert kutokana na kujaza abiria na mizogo kupita
kiasi.Miaka minne iliyopia boto nyingine ilizama na kusababisha vifo vya
watu 70.BBC
No comments:
Post a Comment