Rais Obama akitoa taarifa rasmi baada ya unyakuzi wa Crimea
Mzozo kuhusu Crimea na Ukraine utajadiliwa leo na viongozi wa mataifa mbalimbali akiwemo rais Obama.
Viongozi hao wamejumuika katika kongamano la kujadili usalama wa
nyuklia lakini ajenda hio inatarajiwa kugubikwa na mazungumzo kuhusu
hatua ya Urusi kunyakua eneo la Crimea.
Rais wa Urusi Vladmir Putin amesusia mkutano huo na kumtuma waziri wake wa maswala ya kigeni.
Rais Obama,Waziri Mkuu wa Uingereza David
Cameron na viongozi wenzao kutoka mataifa saba yaliyoendelea zaidi
watakutana katika kikao maalum kuzungumzia hatua zaidi za kuiadhibu
Urusi.
Huenda Moscow ikatengwa zaidi katika maswala ya kisiasa na
kiuchumi.Tayari mataifa ya Ulaya yameapa kuiwekea Urusi vikwazo vya
kiuchumi.BBC
No comments:
Post a Comment