Pages

Sunday, May 25, 2014

VIOJA DUNIANI......KAHABA MKONGWE UINGEREZA ASEMA BADO ANAMVUTO

                        Bi Vogel-Couple kahaba mkongwe zaidi nchini Uingereza

Katika Umri wa miaka 85, Sheila Vogel-Coupe ni kahaba mkongwe zaidi nchini Uingereza na kwa umri huo bado anaweza kutengeneza Pauni 250 kwa saa moja kwa kazi yake.


Miaka minne baada ya kifo cha mume wake wa pili , Vogel-Coupe aliingia katika ukahaba ,kutokana na anachosema ni ukiwa anaosema ndio sababu ya kumfanya ajiingize kwenye biashara hiyo.

Akiwa na uwezo wa kuwaburudisha wateja angalu 10-kwa wiki , ameweza kukutana na wateja wengi kuliko unavyoweza kufikiria.

Akizungumza kuhusu wateja wake wa kiume, alisema : "kuna kitu wanachokiona kwangu. Ni hisia nzuri. Nafahamu nina mvuto sana."

Akiwa amevalia sketi fupi (kimini) na viatu vyenye kisigino kirefu, Vogel-Coupe alijisifu na kujivunia kwamba bado anaweza kutengeneza pesa kutoka chumbani kwake.

Akielezea kwa nini ameamua kuifanya kazi hiyo, alisema: " Sababu ya muhimu zaidi ni kwamba napenda ngono. Hata kuifikiria tu inanifanya nijihisi vizuri''

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mirror, Sheila atakuwa kwenye makala maalum yanayoangazia wanawake wakongwe makahaba 'My Granny the Escort'.
Onyesho hilo litaangazia pia wanawake watatu makahaba walio vikongwe zaidi nchini Uingereza.BBC


No comments:

Post a Comment