Pages

Sunday, May 25, 2014

SOMA HABARI KWA UFUPI

Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), ulioanzishwa wakati wa Bunge la Katiba, umekuwa mwiba kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndani na nje ya Bunge, Tanzania Daima Jumapili limebaini.
Tayari umoja huo unaoundwa na vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi, umeshaweka wazi dhamira yake ya kusimamisha mgombea mmoja katika ngazi tofauti kwenye uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwakani.


 Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa francis ameutaja mzozo kati ya Palestina na Israel kama usiokubalika huku akizitaka pande zote mbili kufanya maamuzi ya busara ili kuweka amani.
Akizungumza mjini Bethlehem ,papa Francis ametaka kubuniwa kwa taifa huru la Palestina pamoja na Israel.
Aidha alifanya maombi katika eneo ambalo Yesu anadaiwa kuzaliwa.

Raia wa Ukraine wanashiriki katika uchaguzi wa urais nchini humo uliotajwa kuwa muhimu katika historia ya taifa hilo.Hatahivyo haijulikani iwapo uchaguzi huo utafanyika katika maeneo mengine ya Ukraine ambapo wanamgambo wanaounga mkono Urusi wanadhibiti maeneo hayo.Maafisa wa uchaguzi katika mji wa mashariki wa Donetsk wameiambia BBC kwamba hakuna vituo vya kupiga kura katika eneo hilo.

Serikali ya jeshi nchini Thailand imewataka wahariri wanane wa magazeti nchini humo kufika mbele yake baadaye hii leo.Mwandishi wa BBC mjini Bangkok amesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kuwa majadiliano ya upande mmoja kuhusu walivyoripoti habari za mapinduzi ya wiki iliopita.



No comments:

Post a Comment