Papa Francis akiomba karibu na ukuta unaotenganisha Bethlehem na Jerusalem.
Mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Francis, amewasili Roma
baada ya kukamilisha ziara yake ya siku tatu Mashariki ya Kati ambapo
alisema kuwa tabia ya baadhi ya mapadri Wakatoliki waliokuwa
wakiwanyanyasa watoto wadogo kingono kanisani inaweza kulinganishwa tu
na misa ya Mashetani.
Baba Mtakatifu alifanya ziara ambayo
ilihudhuriwa na maelfu ya watu wa imani tofauti katika eneo hilo na
wachambuzi wengi wamesema kuwa imekuwa ya kufana.
Wengi wanasema kuwa Baba Mtakatifu kulinganisha vitendo vibaya vya
ngono walivyofanyiwa watoto na mapadri na misa ya mashetani ni lugha
nzito hasa ikitambuliwa kuwa tayari Papa Francis amewahi kuomba msamaha
kwa vitendo hivyo kote duniani.
Vitendo hivyo vimeharibia sifa Kanisa Katoliki kwa muda mrefu sasa.
Taarifa kutoka makao makuu ya Papa yanasema kuwa
kwa mara ya kwanza tangu yeye achukue wadhifa wake anatarajiwa kukutana
na wale walionyanyaswa na mapadri kingono.
Wakatoliki wengi walikasirishwa na vitendo hivyo
na wamefurahi kuwa Papa anaweza kuomba msamaha na kisha akutane na
walioathirika na wengi wanasubiri kusikia atakachowambia atakapokutana
nao.
Hata hivyo iwapo Papa anataka kuaminiwa zaidi
itabidi awaadhibu wanaume waliofanya vitendo hivyo na wale Kanisani
waliokuwa wakiwaficha waliofanya makosa hayo wanapaswa kuachishwa kazi
Kanisani.
Papa anaweza kujivunia ziara yake Mashariki ya
Kati kwa kuwa alipoanza alisema ziara yake ingekuwa ya
Dini na wala sio
siasa. Ni dhahiri kuwa katika Mashariki ya Kati ni vigumu kufahamu kule
siasa zinakoanzia na Dimi kumalizika.
Kwa mfano uamuzi wa Papa kusimama kando ya Ukuta
uliojengwa na Israil kutenganisha Bethlehemu na Jerusalem kumemwingiza
katika siasa kwa sababu ukuta huo ni ishara kamili ya utengano na siasa
zinazotenganisha Wayahudi na Wapalestina.
Ni wazi kuwa wakati huu Papa anafahamu mengi kuhusu siasa za Mashariki ya Kati kama anavyofahamu maswala ya Dini.BBC
No comments:
Post a Comment