Kuna kila dalili
kwamba homa ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Maji na ile ya Nishati na
Madini inazidi kupanda na jana wabunge wa CCM walikutana kwa dharura ili
kunusuru bajeti hizo.Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinasema, Waziri Mkuu
Mizengo Pinda aliwatangazia wabunge hao kuwa Serikali imekubali kuiongezea
Wizara ya Maji Sh100 bilioni kufidia pengo la Mwaka wa Fedha 2013/2014.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema ataipa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) jukumu la kuchunguza
ufisadi wa mamilioni ya fedha katika ununuzi wa tiketi za safari za nje za
wizara yake.
Hatimaye
tume ya uchaguzi nchini Malawi imesema itatangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa
nchi hiyo kesho ijumaa.Uamuzi huo unakuja baada ya mivutano na mapingamizi
kadhaa kwenye mahakama kuu nchini humo.
Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayesimamia Haki za Kibinadamu,
Navi Pillay, amejiunga na maelfu ya watu duniani wanaoshutumu vikali mauaji ya
mwanamke Mpakistani aliyepigwa mawe hadi kufa nje ya mahakama na wanachama wa
familia yake kwa madai ya kuolewa na mwanamume aliyempenda.
Shirika
la fedha duniani IMF leo linazindua kongamano la ngazi ya juu kuzungumzia
maswala ya ukuaji wa Uchumi barani Afrika.Kikao hicho kwa jina "Africa is
rising" kitafanyika katika mji mkuu wa Msumbiji, Maputo.
No comments:
Post a Comment