Pages

Thursday, May 29, 2014

MUME WA FLORA MBASHA ASAKWA KWA TUHUMA ZA UBAKAJI

JESHI la Polisi Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam linamsaka kwa udi na uvumba Emmanuel Mbasha (pichani) ambaye ni mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha kwa madai ya kumbaka shemeji yake mwenye miaka 17 (jina tunalo) ambaye ni yatima.
Taarifa zilizopatikana  ndani  ya  jeshi hilo kupitia vyanzo vyetu makini zinadai kwamba mlalamikaji huyo alifika kituoni hapo Jumatatu iliyopita muda wa mchana na kufungua kesi  yenye Kumbukumbu Na. TBT/RB/3191/2014 na ya Jalada  la  Uchunguzi  Na. TBT/IR/1865/2014 akidai  kufanyiwa  unyama  huo kwa siku mbili (Ijumaa na Jumapili)  wiki iliyopita nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga, Dar.
Ilidaiwa  kuwa, Ijumaa iliyopita mlalamikiwa alifanya kitendo hicho sebuleni nyumbani na Jumapili ilidaiwa  alitekeleza ukatili wake huo ndani ya  gari lake  hali ambayo  ilimfanya mlalamikaji kutoa  taarifa  Kituo cha Polisi, Tabara-Aroma jijini Dar.
Iliendelea kudaiwa kuwa, kufuatia maumivu  makali  aliyoyapata mlalamikaji huyo ilibidi  aende  Hospitali ya Amana  na  kugundulika  kuwa aliingiliwa  kimapenzi na kumsababishia michubuko  sehemu za  siri.
HISTORIA YA MLALAMIKAJI
Mlalamikaji ni  kati  ya  watoto  mapacha  waliozaliwa  jijini Mwanza  na mama  ambaye  jina lake  halikupatikana mara moja.
Mama wa mtoto huyo (kwa sasa ni marehemu pamoja na mume wake) akiwa muumini wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God (EAGT) aliamua  kumtoa mtoto mmoja kwa mama  mzazi wa Flora Mbasha kwa lengo la kumlea,  wakati huo mtoto  huyo alikuwa na miezi  mitatu.
Ikaelezwa kuwa, mama wa  Flora alikaa  na  mtoto huyo akimsomesha hadi alipofika darasa la saba ambapo alimkabidhi kwa Flora na kuishi naye hadi  alipofikwa na janga hilo.
Maelezo zaidi yanasema Mbasha aliweza  kufanya  kitendo  hicho  kwa sababu mkewe (Flora)  ameondoka  nyumbani na kwenda kuishi hotelini kwa kile  kilichodaiwa  kwamba kuna ugomvi  mkubwa ndani ya ndoa yao.
Taarifa  zaidi  zinadai kwa sasa Mbasha naye hayupo  nyumbani kwake huku mlalamikaji yuko  Hospitali  ya Amana akiendelea kufanyiwa  uchunguzi  wa  kiafya ili kubaini kama ana maambukizi ya magonjwa ya zinaa au la!
Kwa  upande  wake  mlalamikaji huyo alipopigiwa  simu  juzi kwa  lengo  la  kuthibitisha  kuhusiana  na sakata  hilo  alikiri na kusema  amekwishatoa  taarifa  polisi   kwa  kitendo alichofanyiwa na mwenye nyumba huyo huyo.UDAKU

No comments:

Post a Comment