Serikali-Kila Mchina sasa ruhsa kuzaa zaidi ya mtoto mmoja
Uchina imeanza kulegeza sheria zake za mpango wa
uzazi, na sasa inapiga kampeni yenye lengo la kuongeza angalau watoto
millioni mbili zaidi wanaozaliwa kila mwaka.
Serikali itaongeza wakunga na wahudumu sambamba
na kupanua nafasi hospitalini na kuongezwa idadi ya vitanda na vifaa
nyenginevyo.
Kwa mda mrefu Uchina imeendeleza sera kali ya mpango wa uzazi ya
kulazimu familia kuwa na mtoto mmoja tu huku wanaokiuka wakichukuliwa
hatua kali jambo linaloshutumiwa kimataifa.
Lakini mwaka jana serikali iliianza kulegeza
kamba kwa kusema iwapo mmoja wa wazazi amekuwa mtoto wa pekee katika
familia basi anaweza kuzaa mtoto wa pili.
Japo hatua za awali zilichukuliwa kukabiliana na
idadi kubwa ya watu nchi humo, sasa kumetokea mapungufu ambayo
yanahitaji kusawazishwa.
Wapanga sera wamependekeza juhudi hizo za kuongeza idadi ya watoto
zichukuliwe sasa la sivyo Uchina itajikuta na upungufu mkubwa wa nguvu
kazi za vijana,huku idadi ya wazee na wanaostaafu ikiwa kubwa kiasi
chakuzorotesha uchumi wa taifa hilo kubwa duniani.Japo bado umaskini
unakumba baadhi ya raia wake,Uchina imepata mafanikio makubwa ya
kiuchumi mnamo siku za hizi karibuni na sasa ndilo taifa la pili
kwa
utajiri duniani,baada ya Marekani.
Hatua hiyo mpya pia huenda ikaleta afueni kwa wengi kwani sera hiyo ya mtoto mmoja kwa familia ilikabiliwa na changamoto nyingi.
Visa na mateso kwa baadhi ya wazazi na watoto
huripotiwa huku watoto vilema, wagonjwa au wa jinsia isiyopendelewa na
wazazi wao kubaguliwa na kutelekezwa.BBC
No comments:
Post a Comment