Kashfa
ya ufisadi wa dola za Marekani milioni 122 (sawa na sh. bilioni 200) katika
akaunti ya Escrow ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imewaweka njia panda vigogo wa
Serikali wanaotuhumiwa kuhusika kufuja fedha hizo, na sasa baadhi yao wamefikia
hatua ya kutajana kama njia ya kukwepa mkono wa sheria.
Mkazi wa
Kigamboni, Baraka Mashauri (27) amedai kupigwa risasi katika mguu wake kulia na
askari polisi wa kituo kidogo cha Gymkhana, jijini Dar es Salaam.Akizungumza na
Tanzania Daima kuhusu tukio hilo, Mashauri alisema lilitokea Mei 17 mwaka huu,
saa saba mchana akiwa katika mtaa wa Shaban Robert akipata chakula karibu na
Mgahawa wa Holiday White akiwa na mwenzake aliyemtaja kwa jina la Musa Mohamed.
Watafiti wa Marekani wamebaini miili
ya watoto hao hutoa viini vya kinga ambavyo hushambulia wadudu wanaosababisha
Malaria.Kwa kumdunga mtu sindano yenye viini hivyo vyo mtu anaweza kukingwa na
ugonjwa huo.Watafiti hao ambao walichapisha matokeo yao kwenye jarida la
kisayansi , wanasema majaribio ya utafiti huo katika binadamu na katika sokwe
sasa yanahitaji kutathminiwa kikamilifu ili kupata matumaini halisi ya chanjo
ya malaria.
Baraza
la usalama la umoja wa mataifa hatimaye limeidhinisha kuwekewa vikwazo kundi la
Boko Haram baada ya utekaji nyara wa takriban wasichana 300 wa shule katika
eneo la Chibok Nigeria.Kundi hilo limeshutumiwa kuwaua maelfu ya watu nchini
Nigeria katika miaka michache iliyopita.
No comments:
Post a Comment