Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana
kilizindua mkakati wake wa ushindi “Hakuna kulala, hakuna kula mpaka kieleweke”
katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kwa kufungua mafunzo yatakayoendeshwa nchi nzima
kwa viongozi wa vyama na Serikali za Mitaa
Mamlaka ya Udhibiti
wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imepunguza nauli za mabasi ya
mikoani huku ikitangaza kubaki kama zilivyokuwa, zile za daladala baada ya
ukokotoaji wake kuonyesha tofauti ndogo ya punguzo kulinganisha na viwango vya
sasa.
Kumekuwa na
mashambulizi zaidi usiku dhidi ya biashara zinazomilikiwa na raia wa kigeni
nchini Afrika Kusini.Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mipira
kutawanya umati kusini mwa mji wa Johannesburg ambapo gari na nyumba vilichomwa
moto.Msemaji wa polisi aliiambia BBC kuwa karibu raia mia mbili wa kigeni
walikimbilia usalama kwenye kituo cha polisi lakini wakaondoka muda baadaye.
Baraza la usalama la
Umoja wa mataifa limetoa kanda yenye ushahidi inayoonyesha matumizi ya gesi ya
chlorine kwenye shambulizi moja mwezi uliopita nchini Syria.Kanda hiyo
inaonyesha watoto watatu walio chini ya miaka minne ambao walikufa licha ya
kuwepo jitihada za kuwakoa.
Viongozi wa vyama
vitano vya upinzani wameshiriki katika mdahalo wa pili wa moja kwa moja ulioandaliwa
na BBC.Katika hoja za kwanza, kiongozi wa chama cha Labour, Ed Miliband,
amesema suala la familia za wafanyakazi atalipa kipaumbele kwanza, wakati
kiongozi wa UK Independence Party,UKIP, Nigel Farage amesema atasaidia biashara
ndogo ndogo.
No comments:
Post a Comment