Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameitaka jumuiya ya albino nchini
kuisukuma Serikali ili Rais Jakaya Kikwete asaini utekelezaji wa hukumu ya
kuwanyonga wauaji wa albino.Kauli ya Lowassa imekuja wiki moja tu baada ya Rais
Kikwete kusema hajapelekewa majina ya watu 16 waliohukumiwa kifo kutokana na
mauaji ya albino kutokana na mlolongo mrefu wa kisheria uliopo kabla ya
kumfikia.
Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Buni Ramole anayewania Ubunge Jimbo la
Moshi Mjini, juzi alitinga mkutanoni na helkopta inayomilikiwa na Mbunge wa
Moshi mjini, Philemon Ndesamburo (Chadema).Ramole alitua na usafiri huo saa
10.37 jioni katika viwanja vya Pasua mjini hapa.
Chama cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) kimemfukuza uanachama Mwanasiasa Mkongwe
Hassan Nassor Moyo baada ya kubainika amekuwa akifanya vitendo vinavyokwenda
kinyume na maadili ya chama ikiwamo kuhutubia mikutano ya hadhara inayoitishwa
na Chama cha Wananchi (CUF) na kukejeli misingi ya Mapinduzi na Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar imefahamika visiwani humo jana.
Waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi ametoa wito wa kufanyika
kikao cha dharura cha viongozi wa umoja wa ulaya kujadili swala la wahamiaji
wanaoangamia kwenye bahari ya Meditarenean wakijaribu kuingia ulaya. Inafuatia
ajali ya hivi punde ambao karibu watu 700 wanahofiwa kufa maji baada ya boti
kuzama baharini kaskazini mwa Libya, kilomita 200 kutoka kisiwa cha Lampedusa,
nchini Italia.
No comments:
Post a Comment