Pages

Friday, April 04, 2014

MBINU ZA CIA KUBADILISHWA MAREKANI

                                             Bunge kufichua siri za CIA

Kamati ya bunge la Marekani kuhusu ujasusi imeidhinisha kuwekwa wazi kwa sehemu mojawepo ya ripoti iliyoiita ya "ukatili" ilioelezea jinsi maafisa wa shiriki la upelelezi la Marekani CIA linavyowahoji wanatuhumiwa wa ugaidi.

Lakini wanakamati wanasema kuwa itachukua muda kabla ya uchunguzi huo kuwekwa wazi kwa umma.
Sehemu ya ripoti iliyofichuliwa inasema kuwa idara ya CIA kila mara ilipotosha serikali kuhusiana na mtindo wake wa kuhoji washukiwa wa ugaidi wakati wa utawala wa Rais George W Bush.
CIA inapinga baadhi ya matokeo ya taarifa hiyo huku ikikiri kutenda matendo ambayo hayakuafikiana na sera za Marekani.

Mwenyekiti wa kamati hiyo ya baraza la Senate Dianne Feinstein anasema matokeo ya kura iliyopigwa kuhusu ripoti hiyo inaonesha wabunge 11-3 waliipigia mswada huo kura huku akisema ni uchunguzi wa matokeo yanayotamausha.
                                            Stakabadhi za CIAkufichuliwa kwa umma

"ripoti hiyo inaonyesha dhuluma inayoenda kinyume na hadhi ya taifa letu,''alisema Dianne
Hii inatia doa historia ya taifa letu na ambayo hairuhusiwi kamwe kufanyika. ''Hivi sivyo wamarekani wanavyofaa kufanya." Mwanasiasa huyo wa chama cha Democrat kutoka Carlifonia amesema.

Taarifa ya wanahabari inasema kuwa japo baadhi ya wanakamati wa chama cha Republican walikashifu ripoti hiyo kwa pamoja na wa Democrats, kulionyesha waziwazi mgawanyiko uliopo ndani ya wajumbe hao.
Matokeo ya uchunguzi huo uliyomo katika kijitabu cha ukurasa 500, yatatumwa kwa Rais Barack Obama ili kuchunguzwa, kutiwa saini, kisha kutolewa kwa umma.BBC

No comments:

Post a Comment