Pages

Friday, April 04, 2014

AFGHANISTAN YAJIANDAA KWA UCHAGUZI

                                               Uchaguzi wa Afghanistan kesho

Vyombo vya usalama nchini Afghanistan viko katika hali ya tahadhari kuu siku moja tu kabla ya uchaguzi mkuu wa urais katika taifa hilo lililosakamwa na vita.

Zaidi ya askari laki mbili wametumwa kote nchini kulinda raiya dhidi ya mashambulizi ya taliban wakitekelza jukumu lao la kikatiba ambalo kundi hilo la kislamu inapinga .
Tume huru ya uchaguzi ya afghanistan imesema kuwa imekwisha wasilisha vifaa vya kupigia kura .

Msemaji wa wa tume hiyo Noor Mohammad Noor, amesema kuwa maandalizi ya uchaguzi yamekamilika.
Wagombea urais wanachini ya saa 12 kukamilisha kampein zao tayari kwa uchaguzi huo utakaoandaliwa kesho.

Mshindi atatangazwa katika raundi ya kwanza iwapo mgombea atasajili takriban asilimia hamsini ya kura zitakazopigwa .
Mkondo wa pili utaandaliwa tu iwapo hakutakuwa na mgombea atakayefikisha asilimia hamsini.

Rais anayeondoka Hamid Karzai hawezi kugombea kwani amekwisha ongoza kwa vipindi viwili.
Viongozi 8 Wanagombea kumrithi rais Karzai ambaye ameongoza tangu mwaka wa 2001 utawala wa Taliban ulipoondolewa mamlakani.

Wagombea wakuu ni Abdullah Abdullah na Zalmai Rassoul, ambao wamewahi kuhudumu kama mawaziri wa maswala ya Kigeni na Ashraf Ghani Ahmadzai ambaye aliwahi kuhudumu kama waziri wa fedha.BBC

No comments:

Post a Comment