Pages

Thursday, April 03, 2014

WEMA AZUA TIMBWILI GLOBAL

Wema Isaac  Sepetu aliyewahi pia kuwa miss Tanzania mwaka 2006 amejitoa fahamu kwa kupandisha mzuka na kutinga makao makuu ya Kampuni ya Global Publishers,Bamaga –mwenge darn a kuzua timbwili laaina yake kisa kikiwa ni kuandikwa kwa habari zake na mpenzi wake Nasibu Abdul Diamond Platnumz.
Tukio hilo la aina yakelilitokea jumatatu iliyopita kwenye ofisi za Global ambao ni wachapishaji wa magazeti  pendwa Amani,Uwazi,Ijumaa,Ijumaa wikienda,Championi na Risasi ,majira ya mchana kweupe hivyo kufunga mtaa huku wapiti njia wakimzodoa  kwa maneno ya kejeli.
Atinga na wapambe dhaifu 

                                                     Wema akiwa na wapambe wake

Akiwa na kundi la wapambe dhaifu na goigoi wakiongozwa na meneja wake Martin Kadinda waliosimama nje ya Ofisi hizo,Wema alifika kwa upole akionekana mkarimu kwa mlinzi ambapo aliomba kuonana na mwandishi  nguli wa magazeti pendwa ,Imelda Mtema .
Mlinzi alimruhusu kwa vile global ni Mjengo wa mastaa na wasio mastaa,huwa hawakauki kuingia na kutoka kwa mambo mbalimbali.Wema alipofika mapokezi  pia aliomba kuonana na mwandishi lakini tofauti na utaratibu ambapo huwa mgeni akifika anaulizwa kama ana “apointimenti” ili aitwe naemuhitaji ,Wema alipitiliza kwa nguvu hadi chumba chahabari akifuatana na kijana aliyekuwa akimrekodi.Akiwa ndani ya chumba cha habari,Wema aliuliza kwa sauti ya juu na ya kujiamini.Imelda yupo wapi?Nauliza Imelda yupo wapi?
Wema na Imelda
                                      Wema akiwa chumba cha habari Global akiongea na                                                      Imelda ambaye hayupo pichani                                        

Katika kumtafuta kwa macho kwa sababu chumba cha habari ni kikubwa huku akionywa na wahariri kwamba atulize mzuka kasha aeleze shida yake,Wema alimuona Imelda akitoa maelezo kwa mhariri kiongozi wa magazeti pendwa Oscar Ndauka kuhusu habari aliyokuwa ameifuatilia.Cha kushangaza Wema alimfuata Imelda mpaka kwenye meza ya mhariri huyo kasha kuanza kufoka kwa sauti ya juu.
Msikieni wenyewe
Kwanini mnafuatilia maisha yangu?kila siku mnaandikahabari zangu na Diamond .Kwanini Imelda unanindika mimi ni msagaji?

Atulizwa agoma
 
Katika kuhoji huko, mhariri kiongozi alijaribu kumtuliza Wema ambaye alikuwa kama amewehuka: ”‘Wema tuelewane, eleza shida yako kwa utaratibu kwani hakuna ofisi isiyokuwa na utaratibu.”
Pamoja na kuambiwa hivyo bado Wema aliyekuwa ameshika Gazeti la Ijumaa Wikienda toleo la Jumatatu iliyopita, aliendelea kumng’ang’ania Imelda ambaye alikuwa akijaribu kumtuliza:
“Wema twende tukakae pale kwenye meza ya mkutano uwaeleze viongozi wangu tatizo lako. Hiyo stori kuwa wewe ni msagaji mbona haipo, ni gazeti gani?”

Licha ya kupewa mwongozo huo, Wema aliendelea kufoka:
“Hivi mnajua mimi ni chizi? Kwa taarifa yenu mimi ni chizi zaidi ya machizi wote, ohooo!”

Mlinzi atonywa atia timu
Baada ya hali kuwa tete, mlinzi wa geti kuu alipigiwa simu ya mezani na kujulishwa juu ya Wema kusababisha kazi kusimama ambapo alifika haraka tayari kwa kumtoa nje kwa hiyari yake au lazima.
Ndipo kukatokea timbwili kubwa, wapambe wake ‘goigoi’ nao waliingia wakitaka kufanya vurugu ili kumteka mwandishi huyo lakini kikosi imara cha Global kikiongozwa na Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi, Saleh Ally kilijiimarisha na kutuliza fujo hizo huku kikiwa makini kuhakikisha Wema na timu yake hawajeruhiwi hata kidogo.

Wema atumia gazeti kama silaha
 
Katika purukushani hiyo, Wema alionesha udhaifu wa kumudu varangati pale alipotumia gazeti aliloshika kumpiga nalo mwandishi Imelda, jambo lililodhibitiwa kama Waasi wa M23 wa Kongo walivyodhibitiwa na Majeshi ya Umoja wa Mataifa, akatolewa nje.

Mbali na Wema
Ukiachia mbali Wema kutulizwa kwa kutolewa nje kwa nguvu, vijana wake walegevu nao waliwekwa chini ya himaya ya Global kwa kunyang’anywa  kamera ya video iliyokuwa ikitumika kuchukua matukio huku nao wakipigwa picha za kutosha na wapiga picha wetu.

Vita kubwa Wema avua viatu
 
Nje ya ofisi, ‘vita’ kubwa kati ya Wema na walinzi wa Global (alifika mwingine kutoka lindo la mbali) ilizuka ambapo staa huyo alivua vile viatu vyake virefu vya rangi ya bluu bahari na kuanza kumpiga navyo mmoja wa walinzi hao akiamini anamkomesha lakini pia akadhibitiwa!

Wema akiwa anarandaranda kwenye geti kuu akiwa peku, alidondosha matusi ya nguoni ambayo hayaandikiki gazetini kwa namna yalivyokuwa makali. Ilikuwa si rahisi kuamini kuwa yeye ni kioo cha jamii.
Timbwili la Wema na wapambe wake akiwemo Petit Man, ambao hawakufua dafu kwa walinzi na vijana wa Global nje ya ofisi hizo, lilichukua zaidi ya nusu saa huku likikusanya kadamnasi na kusababisha mtaa kujifunga wenyewe.

Polisi hao
Hata hivyo, uongozi wa Global uliwasiliana na Polisi wa Kituo cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar ambao walifika na kumkuta Wema na timu yake wakiwa wamepoa mlangoni, wakaambiwa timbwili limetulia hivyo wakatimua zao.

Akapewa Camera kadi noooooo!
Baadaye Wema aliomba kupewa kamera yake ambapo zoezi hilo lilifanyika lakini ‘memori kadi’ yenye picha walizoanza kurekodi, ilitolewa ili kupisha maridhiano kwanza. Waliambiwa kadi hiyo ilitolewa kwa sababu walirekodi bila idhini au kibali cha Kampuni ya Global.

Wema kagoma kuondoka
Baada ya kugundua kadi ya kamera ipo chini ya ulinzi wa Global, Wema alitaka kulianzisha tena akidai hawezi kuondoka hadi apewe kadi hiyo lakini uongozi uliweka ngumu. Baadaye aliondoka kimyakimya. Wakati huo wapambe wake walishaondoka kitambo.

Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, kadi ya kamera hiyo bado ilikuwa inashikiliwa na uongozi wa Global ili kumthibitishia Wema kuwa hawezi kufanya umafia wowote dhidi ya waandishi wa kampuni hiyo yenye nguvu kihabari nchini Tanzania.

Kwa nini?
Kwa mujibu wa Wema, magazeti ya Global yamekuwa yakimwandika vibaya yeye na mpenzi wake Diamond huku akitolea mfano wa habari iliyomhusu yeye na mwigizaji Aunt Ezekiel baada ya kunaswa kwa picha zao zilizoashiria vitendo vya usagaji.Kwa hisani ya GLOBAL

ATULIZWA, AGOMA
Katika kuhoji huko, mhariri kiongozi alijaribu kumtuliza Wema ambaye alikuwa kama amewehuka: ”‘Wema tuelewane, eleza shida yako kwa utaratibu kwani hakuna ofisi isiyokuwa na utaratibu.”
Pamoja na kuambiwa hivyo bado Wema aliyekuwa ameshika Gazeti la Ijumaa Wikienda toleo la Jumatatu iliyopita, aliendelea kumng’ang’ania Imelda ambaye alikuwa akijaribu kumtuliza:
“Wema twende tukakae pale kwenye meza ya mkutano uwaeleze viongozi wangu tatizo lako. Hiyo stori kuwa wewe ni msagaji mbona haipo, ni gazeti gani?” - See more at: http://www.makorokocho.co/2014/04/wema-azua-timbwili-global-ajiita-yeye.html#sthash.JNuaU4li.dpuf

No comments:

Post a Comment