Wanaharakati wakiwa wamebeba maiti ya mmoja wa waandamanaji
Tume ya Uchunguzi ya serikali ya Ukraine imebaini
kuwa polisi wa kikosi maalum cha Ukraine wamedaiwa kuwaua watu kadhaa
walioipinga serikali ya nchi hiyo mjini Kiev mwezi Februari mwaka huu.
Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Arsen Avakov
amewaambia waandishi wa habari kuwa polisi 12 wa kikosi hicho cha Berkut
wametambuliwa na watu kati yao tayari wamekamatwa.
Tume hiyo inahusisha maqshambulio hayo katika mtaa wa Instytutska
mjini Kiev, ambako watu 76 waliuawa kati ya tarehe 18-20 Februari.
Miezi kadhaa ya maandamano makubwa yalisababisha kuondolewa madarakani kwa Rais Viktor Yanukovych.
Katika mkutano wa waandishi wa habari, Bwana
Avakov aliwasilisha matokeo ya uchunguzi wa awali wa mauaji ya watu
wengi waliopigwa risasi hali iliyoishtua Ukraine na dunia.
Wengi wa waandamanaji waliuawa katika mtaa wa
Instytutska karibu na kambi kuu ya maandamano katika eneo la
Independence Square - linalojulikana kama Maidan.
Bwana Avakov alitoa maelezo ya kina kuhusu tukio
moja ambalo amelielezea kuwa tume ya uchunguzi imebaini kuwa wanane
kati ya waliouawa walipigwa na risasi kutoka bunduki ya aina moja.
Waziri huyo pia alionyesha picha zikionyesha
mahali polisi wa kulenga shabaha walipokuwa wamesimama na kufyatua
risasi. Amesema idadi ya polisi waliofyatua risasi hizo wametambulika.
Wakati huo huo mkuu wa Idara ya Usalama ya
Ukraine Valentyn Nalyvaychenko amesema askari wa Idara ya Usalama ya
Urusi(FSB) walihusika katika kupanga operesheni hiyo dhidi ya
waandamanaji.
Amesema FSB walipeleka "tani" za vilipuzi kwa njia ya ndege kwenda Ukraine.BBC
No comments:
Post a Comment