Pages

Tuesday, May 20, 2014

SOMA HABARI KWA UFUPI



Taasisi ya Pride Tanzania ambayo ilianzishwa kwa lengo la kutoa mikopo midogo midogo kwa wajasiriamali imetoweka kwenye orodha ya mali zinazomilikiwa na Serikali.Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inasema taasisi hiyo ilianzishwa Mei 5 mwaka 1993 chini ya Sheria ya Makampuni (CAP 212) kwa dhamana.


Wahamiaji haramu 400 raia wa Burundi wamekamatwa na Idara ya Uhamiaji wilayani Ngara, mkoani Kagera kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria na kurejeshwa nchini mwao katika Operesheni Kimbunga iliyofanyika katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Nchi yetu inapita katika kipindi kigumu wakati huu kutokana na ugonjwa wa homa ya dengue ambao awali ulidhaniwa kuikumba Dar es Salaam, lakini sasa umeenea katika maeneo mengi.

Jeshi la Thailand limetangaza kuweka sheria za kijeshi katika juhudi za kurejesha utulivu wakati nchi hiyo imekumbwa na mzozo wa kisiasa kwa muda.Jeshi hilo pia limejitwika nguvu nyingi zaidi ili kuweza kutekeleza sheria hiyo.

No comments:

Post a Comment