Raia wa Malawi wanafanya uchaguzi mkuu hii leo katika
uchaguzi ambao wagombea kumi na mmoja wanawania kiti cha urais dhidi ya
rais Joyce Banda.
Bi Banda - ambaye aliingia madarakani miaka
miwili iliyopita baada ya kifo cha rais Bingu wa Mutharika - alipendwa
sana na umma wa Malawi awali , lakini sifa zake zilipungua kufuatia
kashfa ya hivi karibuni maarufu kama Cashgate.
Bi Banda anakanusha kuhusika kwa namna yoyote ile na kashfa hiyo.
Wachambuzi wengi wa siasa nchini humo
wanabashiri kuwa bado yeye ndiye anayependwa na wengi hususan ni
umaarufu wake katika maeneo ya vijijini .
Uchaguzi huo unatarajiwa kuwa na mchuano mkali kuwahi kushuhudiwa katika taifa hilo la Malawi.BBC
No comments:
Post a Comment