Pages

Friday, April 04, 2014

SOMA HABARI KWA UFUPI




Jumuiya ya wanafunzi wa Elimu ya Juu Wanachadema Mkoa wa Iringa (CHASO) wamelaani vikali mwenendo mbovu wa Bunge Maalum la Katiba katika kuendesha na kujadili rasimu ya katiba tangu lilipoanza kwa kuendesha malumbano kila kwenye kikao na wakati mwingine wajumbe kuzomeana na kuacha kujadili mambo ya msingi yanayowagharimu Watanzania mamilioni ya Fedha.

Shirika la Ndege la Air Tanzania limeweka rekodi ya ongezeko la abiria kwa asilimia 57 wiki chake baada ya kupokea  ndege ya kukodi yenye uwezo wa kubeba abiria 50 aina ya CRJ-200 pamoja kuiongezea uwezo wa kuruka kwa wakati kwa asilimia 98.

Kamati ya bunge la Marekani kuhusu ujasusi imeidhinisha kuwekwa wazi kwa sehemu mojawepo ya ripoti iliyoiita ya "ukatili" ilioelezea jinsi maafisa wa shiriki la upelelezi la Marekani CIA linavyowahoji wanatuhumiwa wa ugaidi.Lakini wanakamati wanasema kuwa itachukua muda kabla ya uchunguzi huo kuwekwa wazi kwa umma.
                                                      
Vyombo vya usalama nchini Afghanistan viko katika hali ya tahadhari kuu siku moja tu kabla ya uchaguzi mkuu wa urais katika taifa hilo lililosakamwa na vita.Zaidi ya askari laki mbili wametumwa kote nchini kulinda raia dhidi ya mashambulizi ya taliban wakitekelza jukumu lao la kikatiba ambalo kundi hilo la kislamu inapinga .
                                                     

No comments:

Post a Comment