Pages

Friday, April 04, 2014

WAHUKUMIWA KIFO KWA UBAKAJI INDIA




                                                Maandamano ya kupinga ubakaji

Wanaume watatu wamehukumiwa kifo Mjini Mumbai, India baada ya kupatikana na hatia katika visa tofauti vya ubakaji walioufanya kwa pamoja.Moja ya visa hivyo kilitokea dhidi ya mwandishi mpiga picha aliyekuwa kazini alipobakwa.Uamuzi huo umefanywa chini ya sheria mpya iliyopitishwa ya kuwaadhibibu wanaoendeleza uhalifu huo wa ubakaji.

Sheria hiyo ilipitishwa baada ya kile kisa Delhi kilichoughadhabisha umma cha msichana aliyebakwa na ngege basini na kujeruhiwa vibaya sana.

Wanaume hao walikuwa wameshitakiwa kwa kesi ya kumbaka msichana huyo mwandishi aliyekuwa ameenda kupiga picha kiwanda cha nguo kilichotelekezwa, lakini pia mwanamke mwengine akajitokeza na kutoa ushahidi wa jinsi wanaume hao walivyombaka maeneo hayo hayo mwezi mmoja kabla.

Wahukumiwa hao wanaweza kukata rufaa kwa mahakama ya juu zaidi.
Kuongezaka kwa visa vya ubakaji vimepelekea maaandamano ya mara kwa mara nchini humo na sasa mahakama zinaharakisha kusikilizwa kwa kesi hizo.
Pia limekuwa swala la mijadala mikali katika kampeni za uchaguzi unatajariwa hivi karibuni nchini humo.Bbc swahlil

No comments:

Post a Comment