Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu
amesema uchaguzi wa Rais ajaye utakuwa na ushindani mkubwa ndani na nje ya CCM,
huku akibainisha kuwa haogopi mtu kati ya wote wanaotajwa kwenye kinyang’anyiro
hicho, bali anawaheshimu.
Siku tisa baada ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutangaza kumvua uanachama, Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
Zitto Kabwe jana alitinga bungeni na kufanya kikao cha siri na Spika wa Bunge,
Anne Makinda kwa zaidi ya saa moja.
Rais wa Tunisia,
Beji Caib Essebsi, amesema nchi yake imo vitani na ugaidi baada ya wanaume
waliojihami kwa bunduki kuwaua watalii wa kigeni wapatao 17 na raia wawili
katika shambulio katika makavazi mjini Tunis.
China na Japan
wanafanya mkutano wa kwanza wa kiwango cha juu wa usalama katika muda wa miaka
minne.Mkutano huo unaofanyika Tokyo unajumuisha maafisa kutoka wizara za mambo
ya nje na ulinzi.
Wizara ya ulinzi
nchini Marekani imethibitisha kwamba imemuua mojawapo ya viongozi wa kundi la
wapiganaji wa Somalia Al Shabaab kupitia kombora.Adan Garaar alituhumiwa
kupanga shambulio katika jumba la kibiashara la West Gate nchini Kenya miaka
miwili iliyopita.Maafisa nchini Marekani wanasema aliuawa kusini mwa Somalia
ijumaa iliyopita.
No comments:
Post a Comment