Rais Obama anatarajiwa kusisitiza umuhimu wa usalama
Marekani na Ulaya
Rais Obama yuko mjini Brussels ambapo atakutana na viongozi wa muungano
wa Ulaya na shirika la kujihami la NATO, kuzungumzia mzozo wa Ukraine.
Kwenye hotuba muhimu kuhusu sera Rais Obama anatarajiwa kusisitiza
umuhimu wa usalama wa Marekani na nchi za Ulaya na pia kuonya Urusi
dhidi ya kukiuka sheria za kimataifa.
Akizungumza mjini the Hague kabla ya kuelekea
Brussel Rais Obama ameitaja hatua ya Urusi kutwaa eneo la Crimea kutoka
kwa Ukraine kama ishara ya udhaifu.
Hatahivyo amesema bado kuna nafasi ya Urusi kusuluhisha mzozo huo kwa
njia ya amani la sivyo ikabiliwe na vikwazo zaidi vya kiuchumi. Amesema
japo huenda vikwazo hivyo vikaathiri uchumi wa dunia,Urusi ndio
itakayoathirika zaidi.
Mkutano huo pia unatarajiwa kuzingatia maswala
ya kibiashara na pia wasiwasi kwamba Marekani imekuwa ikichunguza kisiri
shuguli za washirika wake kutoka nchi za Ulaya.BBC
No comments:
Post a Comment