Mkakati wa kuwanasua vigogo wa serikali
wanaotuhumiwa kuhusika katika kashfa nzito ya ufisadi wa dola za Marekani
milioni 122 (sawa na sh bilioni 200) katika akaunti ya Baraza la Usuluhishi la
Migogoro ya Kibiashara (Escrow) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), umeanza
kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Victorious la mjini
Moshi, Sixbert Mkelemi, amesema hivi sasa viongozi wa dini wanafanyiwa upekuzi
katika viwanja vya ndege tofauti na miaka ya nyuma kutokana na kupoteza
uaminifu.
Unapouzuru mji wa Malindi uliopo
kwenye mwambao wa Kenya unaonekana kama paradiso.Hata hivyo mji huu ni kitovu
kilichojificha cha biashara ya ngono ya watoto Watoto wadogo wenye umri wa
miaka hata 12 hutumiwa katika ukahaba na filamu za ngono na watalii ambao huwa
tayari kulipa pesa nyingi kwa ajili ya ngono katika maeneo yaliyojificha .
Rais wa Nigeria ametupilia mbali
matakwa ya la kundi la kiislam la Boko Haram kwamba serikali iwaachilie huru
wafungwa wa kundi hilo ndipo litawachilia wasichana zaidi ya 200 waliiotekwa na
kundi hilo.Serikali ya Nigeria imesema iko tayari kwa mazungumzo na kundi la
wanamgambo la Boko Haram.
Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja
amenusurika kifo baada ya kuanguka kutoka orofa ya 11 ya jengo moja mjini
Minnesota Marekani.Vyombo vya habari katika jimbo hilo vimeripoti kuwa Musa
Dayib, amevunjika mkono mara mbili na kwa sasa anapumua kwa usaidizi wa mashine
japo madaktari wanamtarajia kuishi.
No comments:
Post a Comment