Ukisikia jina la Victoria
Beckam,si jina geni kwa wale wapenda burudani,sasa kaa tayari kumuona tena
katika jukwaa la muziki,baada ya kuacha kwa miaka kadhaa.
Victoria ambaye aliwahi kuwa mwanamuziki
wa kundi la spice girls,akiwa katika matembezi ya kawaida nchini Singapore
alitoa burudani ya kwa kupiga kwa umahiri mkubwa piano na kuimba.
Kwa mujibu wa tovuti ya
femalefirst,mwanamuziki huyo alikuwa nyota mpya wa muziki wa pop ukumbini
hapo,kutokana na kuimba na kupiga piano kwa ustadi.
Mwanamuziki huyo alitupia katika ukurasa
wake wa Twitter picha zinazomuonyesha akifanya yake na kuonekana kama
mwanamuziki kinda wakati ana miaka 40,huku akionyesha kila dalili za kutaka
kurudi kwenye fani hiyo aliyoiasi.
No comments:
Post a Comment