Mfanyabiashara
mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi siku ya Ijumaa katika eneo la Mlimani City.
Edson
Cheyo, ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Sowers African iliyopo jirani na Mlimani
City, alifikwa na umauti baada ya kuchukua fedha benki. Inadaiwa baada ya
kutoka benki watu waliokuwa katika pikipiki walimpiga risasi na kuondoka na
fedha zote alizokuwanazo.
Kamati ya Siasa mkoani Mbeya, imeagiza kuitwa kwa
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Bi. Janeth Mbene ili aweze kuhojiwa
akidaiwa kujihusisha na vurugu za kisiasa zinazoendelea katika Wilaya ya Ileje,
mkoani humo.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imesema watu
wawili wamekufa kutokana na ugonjwa wa Ebola, uliolipuka kaskazini-magharibi
mwa nchi hiyo.Hao ni wagonjwa wa kwanza wa Ebola kuripotiwa nje ya Afrika
Magharibi tangu kuzuka kwa ugonjwa huo huko, ingawaje haijaeleweka wazi kama
vifo vya watu hao vinahusiana na mlipuko wa Ebola katika nchi za Afrika
Magharibi.
Maafisa
wa serikali ya Uingereza wanasema kuwa mfanyakazi mmoja wa utabibu kutoka
Uingereza ambaye ameambukizwa virusi vya Ebola nchini Sierra Leone, ataletwa
Uingereza. Atasafirishwa kwa ndege ya jeshi la wanahewa la Uingereza.
No comments:
Post a Comment